Monday, October 31, 2016

YANGA mabingwa watetezi Tanzania bara



Image result for Bossou akishangilia goli

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania bara klabu ya  Young Africans wamerudi dimbani kucheza mchezo wao 12 wa Ligi Kuu sokaTanzania bara msimu wa 2016/2017 wakiongozwa na kocha wao Hans van Pluijm baada ya kufuta mawazo ya kujiuzulu.


Timu ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-0, magoli yaliyofungwa na bekiVincent Bossou, dakika ya 49 na goli kipa wa Mbao FC Emmanuel Mseja akijifunga kwa kushindwa kuzuia mpira uliorushwa na  Mbuyu Twite dakika ya 56, Amissi Tambwe  alikamilisha  idadi magoli mnamo dakika ya 75 na kukamilisha jumla ya magoli 3-0.      


chanzo: manchorypascal.blogspot.com  

DKT. Magufuli kufanya ziara nyengine nje ya nchi

Image result for RAIS MAGUFULI AKIWA SAFFARINI
Kesho October 31 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ataanza ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini Kenya kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.
Rais Magufuli anatarajiwa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi majira ya saa nne asubuhi na baadaye kupokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi ambako viongozi hao watafanya mazungumzo rasmi.
Pamoja na kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais Magufuli atakwenda kutoa heshima katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta na pia anatarajiwa kuhudhuria dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta Ikulu Jijini Nairobi
Katika ziara hii Rais Magufuli anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha Eldoville kilichopo Karen Jijini Nairobi, na pia anatarajiwa kuzindua barabara mchepuko ya Southern By-pass iliyopo Jijini Nairobi.
Barabara hiyo mchepuko ya Southern By-pass ni moja kati ya miradi mikubwa ya barabara nchini Kenya, inaunganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi kwa barabara za juu na chini na imejengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika Jiji hilo. Rais Magufuli anatarajiwa kumaliza ziara yake tarehe 01 Novemba, 2016 na kurejea Jijini Dar es Salaam.

MISS TANZANIA 2016 ATOA YA MOYONI

DIANA LUKUMAY MSHINDI WA MISS TANZANIA 2016.
Baada tu ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la Miss Tanzania mwaka 2016, Mrembo Diana Lukumay alianza kupokea msg za taarifa zilizosambazwa mitandaoni kuonyesha kwamba alifeli kidato cha nne lakini pia pamoja na hayo bado CV yake ilionyesha anayo degree.
Diana ameamua kuweka kila kitu wazi kwa kusema ‘Jina langu ni Diana Loi Lukumay, mmasai na umri wangu ni miaka 18, nilizaliwa Arusha Mount Meru Hospital na ni mtoto wa tatu kwenye familia ya watoto wanne’
3x6a0496
‘Nilisoma shule ya msingi ya serikali Levolosi 2005-2011, sekondari ya kutwa ya serikali Arusha 2012 -2015,  matokeo ya kidato cha nne nilipata darala la pili… nilichaguliwa kujiunga na kidato cha tano mchepuo wa Sanaa kwenda shule ya Wasichana Bwiru Mwanza’
‘Kwakuwa nilikua tayari nipo kwenye tasnia ya urembo niliamua kutojiunga na masomo hayo kwakuwa yalishaingiliana na ratiba za mashindano haya katika ngazi ya kitongoji ambapo nilijiunga na kambi ya Miss Ubungo 2016/2017) – Dian
‘Baada ya kuahirisha masomo ya kidato cha tano niliomba kujiunga na masomo ya ngazi ya cheti kozi ya maswala ya kodi katika chuo cha usimamizi wa fedha ambapo mpaka masomo yanaanza mwanzoni mwa October 2016 tayari nilikua kwenye kambi ya Miss Tanzania, mafanikio ambayo niliyapata baada ya kuibuka mshindi na kutangazwa kuwa lete Raha Miss Kinondoni 2016/2017’
‘Juhudi zangu hazikuishia hapo, nilipotangazwa mshindi sikubweteka na taji hilo bali niliendelea na kazi zangu za kijamii katika jamii yangu ya kimasai.

source: Millardayo.com