YANGA mabingwa watetezi Tanzania bara
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania bara klabu ya Young Africans wamerudi dimbani kucheza mchezo wao 12 wa Ligi Kuu sokaTanzania bara msimu wa 2016/2017 wakiongozwa na kocha wao Hans van Pluijm baada ya kufuta mawazo ya kujiuzulu.
Timu ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-0, magoli yaliyofungwa na bekiVincent Bossou, dakika ya 49 na goli kipa wa Mbao FC Emmanuel Mseja akijifunga kwa kushindwa kuzuia mpira uliorushwa na Mbuyu Twite dakika ya 56, Amissi Tambwe alikamilisha idadi magoli mnamo dakika ya 75 na kukamilisha jumla ya magoli 3-0.
chanzo: manchorypascal.blogspot.com
No comments:
Post a Comment